HUDUMA YA ELISHADAI
Dhamira ya huduma hii ni :
Shalom,
Ni
huduma ambayo ilianzishwa mwaka 2008,
chini ya wanafunzi wa MOA sekondari ikiongozwa na mwasisi na mbeba maono hayo
Mwl. Mrosso AB.
Katika wakati ule ilifanyika kama ni sehemu ya kukutana wanafunzi
wenye kumjua Yesu Kristo ni nani katika maisha yao.
Wakati
ulipo zidi ikawa wenye uhitaji na huduma ni wengi na mchanganyiko wa madhehebu
na dini hivyo huduma iliwapokea kwa
wingi sana na hasa ilikuwa ni mwishoni mwa
mwaka 2009.
Huduma ilipanuka hata kuenea mbali na kuifanya kila leo
kubadilika kutokana na uhitaji wa kiroho hususani katika utendaji wake.
“KUENEZA
HABARI YA UFALME WA MUNGU, na kufanya jamii katika ujumla wake kuwa tayari kwa
saa ile ijayo ambayo yaja kama mwizi''
- UONGOZI KAMILI:
- Mkurugenzi mkuu,
- Katibu mkuu na msaidizi wake,
- Mweka hazina mkuu na msaidizi wake.
- Idara ya Maombi,
- Idara ya Mawasiliano,
- Idara ya Jamii.
Kufikia
August,4,2016 huduma itaweza kufanya shukran mara kumi katika kituo cha watoto
wenye uhitaji.
Tumeanza
kuandaa vitabu mbali mbali vyenye kujenga na kueneza injili kwa sasa kitabu
kimoja kipo tayari,
''TAMBUA NGUVU
ILIYOKATIKA MAAMUZI YAKO JUU YA MAFANIKIO YAKO''
''MILIKI NA
UTAWALE KATIKA KRISTO YESU.''
(Yoshua
1:3 Yeremia 1:10)