Friday 9 August 2013

KANUNI 10 KATIKA SAFARI YA UJANA










Shalom,

KANUNI 10 KTK SAFARI YA UJANA


  1.    Ujana ni zawadi ya pekee sana kwako, Mungu kakupenda, kakupa upeo na kukufanya jinsi ulivyo hata leo.(kujikubali jinsi ulivyo)..”Kwa kuwa ulikuwa wa thamani machoni pangu, na mwenye kuheshimiwa name nimekupenda……”
  2.    Ujana ulionao na jinsi wewe ulivyoumbwa ni wewe tu wa pekee sana ulivyo machoni pa Mungu. Usitamani kuwa kama kijana mwingine.
  3. Jizoeze kuchukua nafasi za kukaa katika ukimya ili ukutane na Mungu wako, hasa ndani kabisa moyoni mwako, hapo utaonja upendo na huruma yake kwako, ni ili maisha yako yawe upendo na huruma kwa wengine.
  4.    Waheshimu, washukuru na uwaombee daima wale wote waliochangia katika safari nzima ya maisha yako hata ulivyo leo. Wazazi waliokuleta hapa duniani, wale waliokupa ushauri mwema, waliokusaidia hasa wakati wa shida.
  5.     Mruhusu Mungu aongoze maisha yako kwa kumsikiliza.Ili ugundue ni sauti yake Mungu uifuate,(mambo mema)  na hii sio sauti ya Mungu , usiifuate (mambo maovu/mabaya).
  6.      Ishi kikamilifu thamani ya ujana wako sasa na daima. Uupende, uutunze na uutetee ujana wako. Usikubali kitu chochote: giza, mahangaiko,  magumu ya maisha,  uchungu,  visikufanye  uharibu ujana  wako. Rum 8:35, 37.
  7.     Mtangulize Mungu daima katika kila jambo, pia uisikilize daima sauti yake, ili ikuongeze uugundue ni wito gani Mungu anataka uuishi na kumtumikia hapa duniani. Kama ndoa, upadre, utawa, ualimu, nk. Naikiwa umeitwa usisite umwitikie kwa ukarimu sana wito huo na uuishi kwa furaha.
  8.   Toa shukrani kwa Muumba wako daima, kwa kuwa amekujalia muda huu wa ujana. Ni vema ukagundua na kutumia vizuri vipaji au mathalani kipaji yeye alivyokujalia/alichokujalia. Ili uzidi kuwa chumvi ya ulimwengu katika mazingira unayoishi kila siku.” Ninyi ni chumvi ya dunia; lakini chumvi ikiwa imeharibika itatiwa nini hata ikolee? Haifai tena kabisa, ila kutupwa nje na kukanyagwa na watu.”  Mt. 5:13
  9.   Usiwahukumu na kuwalaani wale wanaokufanya uonje magumu katika safari ya maisha yako hapa duniani.Maana hata wao wanayo magumu mengi ktk maisha yao, na mara nyingine wanashindwa  kuyabeba na unatupiwa wewe. Wasamehe na kuwaombeadaima. (“Usishindwe na ubaya, bali ushinde ubaya kwa wema.”  Rom. 12:21
  10.    Ujana ni hazina ya pekee, kwa familia,kanisa, na taifa kwa ujumla.Hivyo ni jambo la kumshukuru Mungu  kwa uhai aliokupa, akili njema, elimu uliyonayo ya kutambua meme na mabaya na vipawa vyote alivyoweka  ndani  yako. Haya yote yakusaidie kudhamini uthamani wa ujana wako, na kumpenda zaidi Mungu baba, aliyetuweka hapa duniani tu wasafiri.


    SMS:
    “Hatimaye mzidi kuwa hodari katika Bwana, na katika uweza wa nguvu  zake. Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za shetani.  Efe. 6:10-11.


1 comment:

Anonymous said...

NMEZIPENDA HIZI KANUNI ZA UJANA MBARIKIWE