Monday 4 March 2013

KUENEZA NENO LA MUNGU KWA NJIA YA VITABU

TEMBELEA HAPA="(BONYEZA HAPA)"
 Joseph D. Moriah

SHALOM,

Huduma ya Elishadai imeandaa machapisho ya kitabu kwa ajili ya kueneza zaidi na zaidi neno la Mungu hata lifike mbali zaidi tena katika mfumo wa kawaida kabisa na chenye kubebeka kiurahisi.

Bado kipo kwenye maandalizi ya kufanyiwa ukaguzi wa mwisho kabla ya kuanza kuchapwa kama kitabu kutoka machaapisho ambapo hapo ndipo itakapo julikana kiasi cha fedha itakayo gharimu kuchapwa kitabu chote.

Hivyo kama tulivyo na nia na lengo moja ya kwamba injili ni lazima imfikie kila mmoja na aamue kuokoka na kumfanya Kristo Yesu kuwa bwana na mwokozi wa  maisha yake, hatuna budi kufanya makusanyo kidogo ya hapa na pale ili tuwezeshe kazi hii kwenda kwa wakati.

Tume andaa fomu pamoja na kadi kwa ajili ya michango hiyo ya uchapishwaji wa kitabu, hivyo ni kwa kila mmoja kwa upendeleo wake katika kuchangia. Fomu moja ina nafasi ishirini za kuchangia.

Kuna wengine wapo mbali sana hata wale ambao ni wana Elishadai sasa hapo zimeandaliwa zile simu-bank za M-PESA(vodacom) 0754-312965 na TIGO-PESA 0654-192015 ambazo pia ni namba zinazotumika katika huduma ya Elishadai za kila siku.


Mfano wa fomu za mchango:


Imeandaliwa na Joseph D. Moriah (katibu mkuu)

No comments: