Monday 4 March 2013

MIAKA 4 YA HUDUMA YA ELISHADAI

 A) VIJANA WAKIFUATILIA SIKU HIYO
Siku ya maadhimisho ya miaka 4 ya huduma 14th August 2012. Na hapa ilifanyikia  katika kituo cha watoto na vijana wasio jiweza cha Friennd's of don Bosco-Kimara-Suka Dar es Salaam.

 B)PICHA YA PAMOJA
Hapa tulishiriki na vijana na watoto kwa kila tulichokuwa nacho kwa siku ile pamoja na wao pia kutushirikisha walivyo navyo hususani masuala mazima ya jumbe na sanaa kwa ujumla ilikuwa ni siku ya kupendeza sana kwetu na kwao pia.

 C)MKURUGENZI MTENDAJI WA KITUO(FdB) AKIPOKEA MAPAJI YALIYOPATIKANA SIKU HIYO KUTOKA KWA KAIMU MKURUGENZI WA Elishadai Ministry
Kwa Elishadai kufanya mahudhurio kama hayo si mara ya kwanza kituoni hapo kwani tulipa teuwa pawe sehemu ya kumpa Mungu shukrani zetu pia hivyo tulibeba zawadi kiasi ambazo tulizipata kwa ngugu jamaa marafiki zetu wa karibu.

D)VIONGOZI WA PANDE ZOTE MBILI WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA na mbele ni mapaji yaliyopokelewa.
Tuliambatana na unga wa sembe, sabuni za mche, mashuka, mafuta ya kupikia na wengine walibeba nguo mbalimbali kwa mahitaji ya walivyo ona ni vyema kwao, kwa waliofika kwa mara ya kwanza walipata muamko wa kutaka kufanya hivyo mara kwa mara hususani kipindi kile cha likizo ndefu za mwezi wa sita na mwezi wa kumi na mbili.

E)PICHA YA PAMOJA
Tuna mshukuru sana Mungu kwa kuwa pamoja nasi na kutuwezesha kuyafanikisha hata yale yaliyo juu ya uwezo wetu ila kwa kuwa ni kwa upendo na kutufanya tuweze basi nkdivo hivyo tuliovyo fanikisha katika sherehe hizi za miaka minne ya huduma ya Elishadai.
F)VIONGOZI WA PANDE ZOTE
G)HAKUNA UBAGUZI WA KABILA,UMBILE HATA IMANI WOTE NI WAMOJA
H)NI KWELI NI FURAHA HAINA BUDI NASI TUFURAHI
I)HATA SISI TUPO
J)MGENI KARIBU JISIKIE UPO NASI

Hivyo ndivyo ilivyokuwa siku hiyo Bwana aliyopenda tuiazimishe hivyo picha zipo nyingi nitaendelea kuzituma.


Imeandaliwa na Joseph D. Moriah.  



No comments: