Biblia katika Historia
Biblia ya Kikristo ni mkusanyo wa maandiko matakatifu ya Ukristo. Maandiko hayo mbalimbali yanaitwa tangu zamani sana "vitabu" tu, inavyomaanishwa na neno "biblia" ambalo ni uwingi wa neno la Kigiriki "biblos" yaani "kitabu".
Hutofautishwa
na Tanakh
ambayo ndiyo maandiko matakatifu ya Dini ya Uyahudi na ambayo pengine inatajwa kwa jina
lilelile la “Biblia”,
hasa katika matoleo ya Biblia ya Kiebrania. Vitabu vyake vimo katika
sehemu ya kwanza ya Biblia ya Kikristo kwa jina la “Agano la Kale”.
Biblia ya
Kikristo hugawiwa sehemu mbili ambayo ni Agano la Kale na Agano Jipya. Agano la
Kale lina maandiko yaliyoandikwa kabla ya Yesu Kristo na vitabu vya Agano Jipya
viliandikwa baada yake.
Agano la Kale
Kimsingi vitabu
vya Agano la Kale ni vilevile vya Biblia ya Kiebrania, ingawa madhehebu ya Kikristo hutofautiana kidogo katika
hilo. Ni kwamba wakati wa kutokea kwa Ukristo palikuwa na tofauti ndani ya
Uyahudi kuhusu vitabu vilivyohesabiwa kuwa maandiko matakatifu. Suala hilo
liliondolewa kuanzia mwaka 80 BK wataalamu wa Wayahudi wa huko Jabneh (Jamnia)
walipochukua msimamo mkali dhidi ya wafuasi wa Yesu.
Kwa wakati huo
Wakristo walikuwa wamezoea tayari toleo la Kigiriki la maandiko matakatifu
yaliyotafsiriwa katika karne ya 2 KK ambalo linajulikana kwa jina la Septuaginta
na kuwa na vitabu kadhaa visivyokuwa vimetunzwa katika lugha asili ya Kiebrania
wala ya Kiaramu,
au vilivyoandikwa moja kwa moja katika lugha ya Kigiriki.
Hivyo Biblia ya
Kikristo ilikuwa na vitabu 7 (viwili vya Wamakabayo, Yoshua bin Sira, Hekima, Tobiti, Yudithi,
na Baruku,
pamoja na sehemu za Esta na Danieli)
visivyokubaliwa baadaye na Wayahudi.
Vitabu hivyo 7
vikaja kukataliwa na Martin Luther katika karne ya 16, halafu na Waprostestant wengi, lakini
vinazidi kutumiwa na Kanisa Katoliki na Waorthodoksi kwa jina la Deuterokanoni.
Agano Jipya
Kuna vitabu 27
vya Agano Jipya. Vinne vya kwanza ni Injili nne zinazoleta habari za maisha,
matendo na maneno ya Yesu.
Vingine ni Matendo ya
Mitume, Nyaraka za Mitume, hasa Mtume Paulo,
na Ufunuo
wa Yohane.
INAENDELEA..............................................