Thursday 2 May 2013

MCHUNGAJI




WACHUNGAJI  KATIKA KANISA

MCHUNGAJI

NI  YULE  ANAYECHUNGA, ANAYELIHUDUMIA, NA KULILINDA  KANISA. Katika 1Sam 17:34-37, Math 18:12-14, Yoh 10:12,14, Zek 11:16,17.
Mwokozi wetu Yesu Kristo ni yote katka haya kuhusiana na kanisa la ulimwengu na ushirika wa eneo la wa waamini. Ikiwa tukitilia maanani sifa zake zote na upendo wake,upole, kutokuwa mbinafsi,wema, mwenye utaayari  wake wa kukubali kukataliwa,kudharauliwa, aibu, mateso.
Ni mfano wa namna gani.?, alikufa kutuoka sisi, anaishi kututunza na katika kurudi kwake atuchukue twende kwake. Katika  nuru ya mfano huu mkamilifu tunahitaji kuiangalia Biblia mwongozo waetu wa kipekee  unavyotuambia  kuhusu kinachohitajika kwa wachungaji katika kutawala, utaratibu na utiifu katika kusanyiko la eneo.

NI NANI ALIYEWACHAGUA WAZEE.?

(WAANGALIZI AU MAASKOFU)


Katika Mdo 20:28 inataja wazi kuwa  Roho Mtakatifu “….amewaweka nyinyi kuwa waangalizi ndani yake….” Pamoja na mamlaka yao ya kipekee ya  kitume na ufahamu wa ndani wa kiroho waliwachagua(
Waliwaekea mikono)wazee katika kanisa la kwanza kwa  njia ileile waliobariki mafundisho  kwa ajili ya kanisa ulimwengu na la eneo( Mdo 14:23, 16:4 ) Haya yalifanyika chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu haikufanyika kupitia uchaguzi holela, kura au kuteuliwa kwa ngazi za kiutawala wa kidini, bali zoezi la  kiroho na kujifunza kwa makini juu ya watu hao, kama tunavyoona katika ubora  na wasifu unaotakiwa kwao.
Mungu ametupa mafundisho ya mitume kama ilivyodhihirishwa  kwao na Roho Mtakatifu na kuhifadhiwa kwa ajili yetu katika kanuni ya maandiko-neno la Mungu lililovuviwa. Kwa jinsi hiyo , hii ndiyo msingi  pekee wa  kutambua  wachumgaji katikati yetu.
Ni yupi anaye staili kuwa mchungaji, 1Pet 5:2-5, Sifa za wale watu wasiolaumiwa katika haya yaliyo orodheshwa kwa ajili yetu katika 1Tim 3:2-7,


Itaendelea.......................

No comments: