Saturday 4 May 2013

MCHUNGAJI



MAHITAJI:

1.     1.  Awe aliyeoa .   2. Awe na kiasi.(Mwangalifu, mawazo safi.)  3. Awe na busara   4. Awe mtu wa utaratibu (mawazo mazuri, anayejitaawla)   5. Awe mkaribishaji (rafiki kwa wageni)  6. Awe anayejua kufundisha (mwenye ujuzi wa kufundisha mafundisho ya kweli.)  7. Awe mtu asiye zoelea ulvi.   8.  Asiwe mtu wa kushabikia magomvi. 9. Awe mpole  10. Asiwe mtu wa kupenda ubishani.  11.  Mwenye kuitawala nyumba yake mwenyewe.  12. Asiwe mpenda fedha  13. Asiwe mtu aliyeongoka karibuni.(hajakomaa katka maandiko)  14. Anaye shuhudiwa mema na watu walio nje (aliye shaihidi mwema kwa dunia.)
                                                                                                                                 
Katika Heb 13:17 inasema “…watatoa hesabu  kwa kazi yao ya uchungaji ..” Inahitajika kujitoa kiasi kikubwa na kuwajibika.

WAJIBU:

Waangalizi wako chini ya uchungaji wa Bwana Yesu Kristo.Hawa ni watu ambao wanatazamwa na waamini wakati wa magumu, mfadhaiko, huzuni na maumivu. Wanawatazama kwa uongozi, mafundisho na kuelekeza kwa njia ya huduma ya neon na kwa kuwa mifano.Wanatakiwa kujenga nidhamu katika kifungo cha maandiko kuhakikisha utaratibu mzuri na ushuhuda mzuri katika kusanyiko na kuhakikisha kuwa mafundisho potofu hayaingizwi.
Wazee (wachungaji, waangalizi) hawachaguliwi na watu kama vile ilikuwa ni mfumo Fulani unaofuatwa wa uongozi  wa ngazi ya uongozi wa kidini, au kamati teule ya kufanya maamuzi, lakini ni kwa Roho wa Mungu.Wazee wana uzoefu mwingi katika masuala ya familia na juu chini, na masumbufu ya maisha, kwa kawaida wanaweza kuwa na sifa za kuongoza, kushauri, na kufariji wale wenye uhitaji.Petro mtume akijitoa kwa mfano wa mzee anaongelea juu ya wajibu wa wachungaji na utawala wao:1Pet  5:1-5
1.       Kulinda kundi.
2.        Kuongoza (kuwa vielelezo)    

HAKUNA KUJIHUDHULU WALA HAKUNA MUDA WA KUACHA KUWA MCHUNGAJI

Ikiwa anataka kufanya wajibu  kama mchungaji, mzee au mwangalizi basi hakuna kitu kinachopungua kiroho.Wachungaji wa kimungu hawataruhusu kupotoshwa na upinzani, uzushi au mateso ya aina yoyote. Yoh 10:12-13, Bwana anaongelea wachungaji wa aina mblli toofauti. Waangalizi, wazee angalieni ;nia zenu , je mnafuata mfano wa mchungaji mwema.? 

 

"MWENYEZI MUNGU AWABARIKI NA KUWAZIDISHIA HAJA ZA MIOYO YENU KATIKA WEMA WAKE" 

 

AMEN.

No comments: