Tuesday 16 April 2013

YALIYOJIRI KWENYE SEMINA YA VIJANA



SHALOM,


REPOT YA SEMINA ILIPOFANYIKIA SEMINA YA VIJANA JUMAMOSI YA TAREHE 13 APRIL 2013,
MKONO WA MUNGU ULITENDA KAZI YAKE TENA PASI KUJIFICHA KWANI VIJANA WALIJITOKEZA KWA WINGI TENA KWA MUDA TIMILIFU.

SOMO 1:  “FUNGUO NANE ZA KUFANIKIWA  KIHUDUMA.”

NA MCH. PROSPER K. NTEPA.
WAKOLOSAI 4 : 17


MAMBO 4 YENYE MAANA KATIKA SOMO HILI

+ KUJUA KARAMA AU HUDUMA ULIYOITIWA.
+ WATU WENGINE WAWEZE WAJUE HUDUMA ULIYONAYO.
+ KUWA MWANGALIFU NA HUDUMA ULIYOPEWA.
+ UWE MWAMINIFU KUFUATILIA ILE HUDUMA AU KARAMA ULIYOITIWA. 


                  KWAYA YA VIJANA IKIBURUDISHA WAKATI WA SEMINA

YA KUZINGATIA ILI UFANIKIWE KATIKA HUDUMA

  •   NI RAHISI KUTUMIKA WAKATI WA UJANA TOFAUTI NA UZEENI,
  •   MAISHA SI MAANDALIZI YA KIMWILI TU BALI NA KIROHO PIA
  •   UJUE KILA MTU ANAYO KARAMA LAKINI SI WOTE WANAO ZIJUA KARAMA WALIZONAZO,
  •   HUWEZI KUFANIKIWA KATIKA HUDUMA USIYOIJUA.
 NB:  “MAFANIKIO YA HUDUMA HAYALINGANISHWI NA HUDUMA NYINGINE KWANI KILA HUDUMA INA WITO WAKE KWA UPEKEE WAKE.”


TUKUTANE KWA MWENDELEZO WA SOMO HILI HAPO KESHO NA TUZIONE FUNGUO ZA MAFANIKIO YA HUDUMA.
BARIKIWA. 

No comments: