Friday 9 August 2013

KIJANA USIKUBALI KUWA MTUMWA WA SHETANI

Shalom,

Kijana ni hima sasa ukawa ni kiongozi na mvuvi wa kuvua watu kutoka kutokuamini hata wawe waamini, kwa kuwa Mungu amekupa tayari nguvu na uweza wa kipekee sana hususani katika suala zima la kiutendaji. Na tarajia kukuona unachukua hatua madhubuti katika kufanya mabadiliko ya kimwili, kiroho na kiakili ili uweze kukua kwa kila idara na kuvitambua vipawa na karama zilizo ndani yako ikiwa ni tayari hata uanze kuvitumia vipawa hivyo na karama hizo kwa utumishi wa Mungu hata daima.

2Timotheo 3:1-5.

"Lakini ufahamu neno hili, ya kuwa siku za mwisho kutakuwako nyakati za hatari.
 Maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kutukana, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio safi,  wasiowapenda wa kwao, wasiotaka kufanya suluhu, wasingiziaji, wasiojizuia, wakali, wasiopenda mema,  wasaliti, wakaidi, wenye kujivuna, wapendao anasa kuliko kumpenda Mungu;  wenye mfano wa utauwa, lakini wakikana nguvu zake; hao nao ujiepushe nao. "

EL-ROI.

1 comment:

Anonymous said...

Amen